Kutana Na EnGen
EnGen ni jukwaa la kujifunza mtandaoni linalotolewa na Gap Inc. kwa watu wanaotaka kuimarisha ujuzi wao wa Kiingereza. Kushiriki katika EnGen ni kwa hiari na hakukusudiwa kukupa mafunzo ya kazi. Unaweza kutumia jukwaa bure kwa masaa 24/7 kwa kompyuta, kompyuta kibao au simu yako ya mkononi. Jukwaa hili linazingatia kasi ya mtu binafsi kwa hiyo unaweza kudhibiti ratiba yako mwenyewe, na kupitia maudhui yanayofaa kwa malengo yako ya kibinafsi na ya kitaaluma ya kujifunza Kiingereza.
Jisajili kwenye EnGen

Wanafunzi wa EnGen wanafikia malengo yao ya lugha
“Sihitaji tena mtafsiri ili niwasiliane na wafanyakazi wenzangu na marafiki.”
- Mwanafunzi wa EnGen

Programu ya EnGen
Inatoa cheti cha kukamilisha kozi na udhibitisho wa kiwango chako cha Kiingereza.
Jukwaa La EnGen + Mafunzo ya Kikundi
Utaweza kutumia jukwaa kwa miezi 6. Hii inajumuisha kufanya mafunzo 8 ya kikundi kwa mwezi, moja kwa moja kwa kompyuta, kompyuta kibao, au kifaa chako cha rununu. Mafunzo haya yameundwa kulingana na kiwango chako cha ustadi. Pia utaweza kutumia jukwaa la EnGen lenye maudhui yanayozingatia kasi ya mtu binafsi, mapitio ya msamiati, zana ya mazoezi ya matamshi, na tathmini za ustadi. Mwalimu wa EnGen atakukusaidia kujua jinsi ya kutumia jukwaa, kufanya mipango ya kujifunza, na kushiriki. Kushiriki ni kwa hiari kabisa na hakukusudiwi kukupa mafunzo ya kazi.
Anza kwa Hatua 3 Rahisi
①
Jifunze kuhusu EnGen kwa kupitia taarifa katika ukurasa huu. Tafadhali rejelea maswali yanayoulizwa sana hapo chini ikiwa bado una maswali kuhusu kuanza.
②
Mara tu unapokuwa tayari kujiandikisha, jaza fomu ya usajili iliyo hapo chini.
Kujaza fomu ya usajili kunamaanisha kuwa unaomba kujiandikisha kwenye jukwaa na unajitolea kutumia jukwaa kila wiki. Kukiwa na nafasi, utaandikishwa kiotomatiki baada ya kujisajili.
③
Baada ya kuwasilisha usajili wako, angalia barua pepe yako ili upate taarifa kuhusu hatua zinazofuata!

Jinsi ya Kufanikiwa
Jifunze kwa Masaa 2-3 Kila Wiki
Ni muhimu kujifunza mara kwa mara na kushiriki ili uone maendeleo katika ujuzi wako wa Kiingereza.
Hudhuria Mafunzo ya Kikundi
Hudhuria mafunzo 2 ya mtandaoni kila wiki ili ufanye mazoezi ya ustadi wako wa kuzungumza.
Chunguza Katalogi
Pata maudhui kwenye katalogi yako yanayolingana na malengo yako ya kujifunza Kiingereza ili yakupe motisha na yakusaidie kushiriki.
Soma Barua pepe Zako za Maendeleo
Utapokea barua pepe kila Jumapili pamoja na maendeleo yako na vidokezo vya nini cha kufanya baadaye. Hii itakusaidia kuendelea kufuata mpango wako wa EnGen.
Shiriki Katika Vikao vya Mafunzo ya Kikundi
Utaalikwa kwenye vikao vya mafunzo ambapo utajifunza kutumia jukwaa, kutumia katalogi, kuzungumza kuhusu malengo yako, na kupata majibu ya maswali yako.
MASWALI YANAYOULIZWA SANA
-
Hapana, Gap Inc. inafurahi kukupa jukwaa la EnGen bure.
-
Jaza tu fomu ya usajili inayopatikana kwenye ukurasa huu na hii itatujulisha kuwa uko tayari kuanza kujifunza Kiingereza!
-
Ili ushiriki katika programu lazima uwe mfanyakazi wa Gap Inc. katika Fishkill au Groveport CECs na uwe mwanafunzi wa lugha ya Kiingereza. Watakaofika wa kwanza ndio watakaoweza kushiriki.
-
Baada ya kuwasilisha ombi lako la EnGen, tafadhali angalia barua pepe yako kwa maelezo zaidi.
-
Utaweza kutumia jukwaa kwa miezi 6
-
Baada ya kujiandikisha, unaweza kupakua programu yetu ya rununu kwa kutafuta “EnGen” katika duka lako la programu au kwa kutumia kiungo hiki kufikia akaunti yako kwenye kompyuta yako. Kiungo cha EnGen
-
EnGen inabinafsisha programu ya mafunzo ya Kiingereza kwa ajili yako kulingana na kiwango chako, malengo na mambo yanayokuvutia. Unaimarisha ujuzi wako wa Kiingereza kwenye EnGen kwa programu yetu ya simu ya mkononi au kompyuta kwa kufanya masomo mafupi ya ulimwengu halisi yanayohusu maisha yako na yanayokupa motisha na kukusaidia kushiriki.
-
Unaweza kutuma barua pepe kwa help@getengen.com ukiwa na maswali yoyote.